SHADDA NA KIIMBO KATIKA KISWAHILI
SHADDA KATIKA KISWAHILI
A] SHADDA.[sress]
Shadda ni mkazo [kuongeza nguvu katika utamkaji] unaotiwa katika silabi fulani katika neno ili kulipa neno lenyewe maana fulani kusudiwa.
shadda hutumika katika; i]kutofautisha maana ya maneno yenye maendelezo sawa
mifano, 'ala - kifaa
a'la - neno la mshangao
wa'lakini - udhaifu/dosari/unyonge
wala'kini - kumaanisha hata hivyo.
ba'rabara - kumaanisha vyeme ifaavyo na
bara'bara - kumaanisha njia kuu/baraste
ila - isipokuwa
i'la -kasoro
ii]kutofautisha maana ya sentensi na nyingine kwa kuiadhiri kimaaana na shadda
mifano, wazima 'moto - wale wanao zima moto
wa'zima moto - unuzima moto
TANBIHI
Maneno yote ya kiswahili asilia [yenye asili ya kibantu ] huwekwa shadda katika silabi ya pili kutoka mwisho huku yaliyokopwa kutoka lugha zingine yakibeba shadda katika silabi tofauti tofauti.
Silabi iliyowekwa shadda katika maneno ya kukopwa hutambuliwa kwa aidha kidato kinachotumika kuitamka au mda inayochukuwa ikilinganishwa na zingine.kidato chake huwa cha juu na mda mrefu ikilinganishwa na zingine.
Tupatane kwenye makala yafuatayo tukikichambua kiimbo.
Comments
Post a Comment