SILABI ZA KISWAHILI NA MIUNDO YAKE WAZIFAHAMU?

Fasili ya silabi

Zipo fasili nyingi za dhana ya silabi, lakini iliyorahisi  kuhifadhika  kumbukizini haswa katika ngazi ya shule za upili ni kuwa silabi ni tamko kamili katika neno.

Silabi  ni dhana ya kimsingi ya sarufi ya kiswahili, ambayo huwa kipashio na kigezo muhimu katika kubuni na uendelezaji  wa maneno yote ya lugha hii ya waswahili.

Miundo ya silabi

a]Tunaweza kuunganisha konsonanti na irabu kama vile -ma ,-ba,-ta ,-cha na zingine.[KI]

b]Kuunga mwambatano wa silabi mbili na irabu -twa,-yva,-mba,-chwa miongoni mwa zingine.[KKI

ch]Mwambatano wa silabi tatu na irabu -nywa, -njwa,-ngwa,-mbwe na kadhalika. [KKKI]

 d] Irabu pekee -a,-e,-i, -o,-u.[I]

e] Na mwisho konsonanti pekee [k]. Ni muhimu kuegemea kuwa maneno mengi ambayo asili yake huwa sio uswahilini huchukua silabi za konsonanti moja kama vile mu-k-ta-dha, da-k-ta-ri,so-k-si miongoni mwa mengine.

kwa kutumia miundo hii mitano pekee katika kubainisha miundo ya silabi  huenda ikawa hata rahisi kuhesabu na kutolea mifano kwa sababu za kimtihani.

Hivyo,
 K+K+K+I/KKKI
 K+K+I/KKI
 K+I/KI
watahini wametumia hii miundo ya kihesabatihesabati kuwatishia watahiniwa ambao mara nyingi kwa kukosa uelewa wa kimsingi wa miundo ya silabi hukosa taswira ya maumbo kisirabi na kuishia kuwa kitoweo cha watahini.

kwenye ngazi ya shule za upili wanafunzi hupatana na kipashio cha silabi hiki katika:

i] kujibia swali la vipashio yva kimsingi vya lugha ya kiswahili

vipashio hivi ambavyo ni sauti,silabi,neno na sentensi haviwezi kuorodheshwa pasi kutaja silabi.

ii] kutambua miundo ya silabi kwenye maneno au maneno yaliyo na  miundo pewa ya silabi

Mtahiniwa analazika kutafuta miudo yoyote wezekana ya silabi katika ule utaratibu pale kisha mwenyewe abuni neno la kwake na kuziwahi  alama zile kirahisi.



 



Comments

Popular Posts