KIIMBO KATIKA KISWAHILI
KIIMBO [intonation]
Kiimbo ni ile hali ya kupanda au kushushwa kwa sauti wakati wa utamkaji.
Kiimbo ni kiziada cha lugha ongezi ambacho hutusaidia kuelewa maana ya kisawasawa ya kauli mbalimbali na hivyo kutusaidia katika kuzielewa kauli zenyewe kama ni swali,hisia,amri,ombi ama ni maelekezo.
Katika uchunguzi wa kiimbo tunajikita sana katika toni ya usemi wakati wa utamkaji ambayo huwa tofauti kutegemea thamira ya usemi huo.
MAJUKUMU YA KIIMBO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
Kiimbo katika lugha ya kiswahili kina majukumu yafuatayo ambayo yanatokana na toni mbali mbali:
i] Kiimbo cha toni ya kuuliza swali.
ii]Kiimbo cha toni ya kuonyesha hisia/mshangao
ii]Kiimbo cha toni kutoa kauli/taarifa
iv]Kiimbo cha toni kutoa amri
v]Kiimbo cha toni yakutoa rai/kufanya ombi au kusihi.
AINA ZA SENTENSI ZA KISWAHILI KUTOKANA NA KIIMBO
Sentensi za kiswahili kando na kuainishwa kutokana na muundo wake wa kimaneno,zaweza pia kuainishwa kwa kutumia kiimbo.
kutokana na kiimbo tunapata aina zifuatazo za sentensi:
i]Sentesi za swali.
Sentensi hizi huanza kwa toni ya ruwaza [pattern] ya wastani na kisha kupanda pale mwisho.
Sentensi hizi hutambulishwa na kuwepo kwa alama ya swali mwishoni mwa sentensi.
mifano,
Mama ametoka kazini?
Wewe unaandika nini?
Bibiye alishikwa lini?
Umesema waitwa nani?
ii]sentensi za mshangao
Sentensi hizi huanza kwa ruwaza ya juu na kudumishwa.
njia rahisi ya kuzitambua sentensi hizi ni kuwepo kwa alama hisi.
mifano,
Salaala!Mwalimu anafundisha!
Lo! lo!kumbe pia wewe ni mwizi!
Masalaale! wote wamekwisha!
Aka! uliibuka mkia!
TAN. Baada ya alama hisi hamna kikomo na alama hisi hufuatwa na herufi kubwa ikitokea ndani ya sentesi
Tunatumia alama hisi kuonyesha kwamba mnamshangao.
iii]Sentensi za kutoa taarifa/kauli tu.
katika kutambua sentensi hizi kiimbo kinashushwa.
Mwanafunzi anasoma.
Mimi nitapika ugali.
Mama atafika shuleni kesho.
iv] Sentensi za amri
Toni ya kiimbo kinachotumika hapa ni kile cha kutoa maelekezo
Mifano
Ondoka haraka!
Inama upesi!
Enda shuleni!
Fungua dirisha!
v]Sentensi za rai/ombi
Toni ya kunyenyekea na kutaka kuhurumiwa hutawala.
Mifano;
Tafadhari usinipige,
Nipe chakula kidogo'
Naomba usaidizi
Hebu nisaidie chumvi
zoezi
1.mama anaandika.
Iainishe sentensi hii kwa kutumia kiimbo[ Alama 4]
Comments
Post a Comment