SAUTI ZA KISWAHILI NA UTAHINI WAKE

SAUTI ZA KISWAHILI

]Sauti ni nini?

Sauti ni ile hali ya mawimbi hewa kuzuiliwa au kutozuiliwa katika ala mbalimbali za kutamkia kutoka mapafuni hadi midomoni.

Aina za sauti

kuna aina mbili kuu za sauti za kiswahili;
         i] sauti za irabu/vokali
        ii] sauti za konsonanti

Sauti za irabu
Hizi ni sauti ambazo hutamkiwa kwenye chemba cha kinywa pasi hewa kuzuiliwa 
sauti hizi hujumuisha /a/, /e/, /i/, /o/ na /u/.

Muainisho wa sauti za irabu
Katika kuonyesha pale ambapo vokali/irabu zinapotamkiwa,huwa tunazingatia vigezo vitatu vya kimsingi na maalum
                                       i]sehemu ya ulimi ya kutamkia[mbele,kati au nyuma]
                                      ii]muinuko wa ulimi[wa chini,wa wastani au wa juu] na 
                                     iii]mikao ya midomo.
Baada ya kuzingatia haya, mchoro wa pembe tatu[ukichukuliwa kuwa ulimi] hutusaidia kuiweka irabu inapotamkika kwenye kinywa.

            i]/a/ kati[sehemu ya ulimi] chini[muinuko wa ulimi] midomo katandanzwa.

           ii]/e/mbele[sehemu ya ulimi] chini[muinuko wa ulimi]midomo katandazwa

.         iii]/i/mbele[sehemu ya ulimi] juu[mwinuko wa ulimi] midomo 
                 katandazwa.
          iv]/o/nyuma[sehemu ya ulimi] chini[mwinukw wa ulimi] midomo kaviringwa.

           v]/u/nyuma[sehemu ya ulimi] juu [mwinuko wa ulimi] midomo kaviringwa.
zoezi
kwa kutumia mchoro wa pembe tatu ainisha irabu zote za kiswahili.

Sifa za irabu
Sifa za irabu hutokana na vile vigezo maalum vya kuainishia irabu hizo.
a]Ikiwa irabu itatamkiwa sehemu ya mbele ya ulimi ,kati au nyuma,sifa yake itakuwa ni irabu ya mbele,kati au nyuma tawalia.

b]Ikiwa irabu itakuwa na mwinuko wa chini,wastani,au wa juu, sifa yake itakuwa ni irabu ya chini, wastani  au juu mtawalia.

c]iwapo irabu wakati wa kuitamka midomo itaviringwa au kutadazwa,sifa ya irabu hiyo itakuwa ni ya kuviringa au ya kutandaza mtawalia.

zoezi
Eleza sifa za irabu zote za kiswahili

Utahini wa sauti za irabu

Tannbihi: i]lazima irabu iandikwe kwenye mishazari / /
               ii]lazima irabu iandikwe kwa herufi ndogo
watahini hupendelea kuuliza maswali ya mlinganisho wa irabu moja na nyingine na wale wanafunzi wasio tumia viunganishi vya  mlinganisho huishia kutoa maelezo ya pale zinapotamkiwa sauti hizo bila ya kujibu swali ambalo linalenga sifa.
kwa mfano.
                    Tofautisha kati ya sauti/i/ na /o/
jibu sahihi ni /i/ ni sauti  ya mbele ilhali /o/ ni sauti ya nyuma.
                                                    
                      /i/ ni sauti ya kutandaza huku /o/ ikiwa ni sauti ya kuviringa
                       
                      /i/ inasababisha mwinuko wa juu lakini /o/ inasababisha mlalo.


Comments

  1. Somo la kiswahili remain my bae. Asanti Mwalimu Sam kwa maelekezo yako kuhusu sautu na Tamko. Nashkuru

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts