SAUTI ZA KONSONANTI NA MUAINISHO WAKE.
SAUTI ZA KONSONANTI
Utahini wa konsonanti.
Hizi ni sauti ambazo wakati wa kuzitamka, hewa huzuiliwa katika ala mbalimbali za kutamkia.
Ala za kutamkia ni sehemu za mwili ambazo huchukuliwa kama vifaa vya kutamkia ambavyo vipo katika mkondohewa wa kutamkia kutoka mapafuni hadi kwenye midomo na mapua.
Ala hizi ni pamoja na:
midomo,meno,ufizi,kaa kaa ngumu,kaa kaa laini,ulimi,kidakatonge,koo,nyuzi za sauti, umio wa hewa,mapua,nyuzi za sauti na mapafu.
MUAINISHO WA KONSONANTI ZA KISWAHILI
Katika kuainisha sauti za konsonanti tunazingatia vigezo vitatu maalumu kwani vigezo hivi ndivyo hutupa aina za sauti za konsonsti.
i] jinsi hewa inavyo zuiliwa na kuachiliwa
ii]mahali hewa inapozuiliwa
iii]mtetemeko kwenye nyuzi za sauti
kutokana na vigezo hivi tunapata
a]jinsi hewa inavyozuiliwa
i] Iwapo hewa itazuiliwa katika ala/sehemu ya kutamka kisha ikaachilliwa kwa mpigo na mpasuko wa kwapamoja, tunapata sauti za konsonsati za vipasuo.
sauti hizi ni pamoja na /p/,/b/,/t/,/d/,/j/,/k/ na /g/
ii]ikiwa ala za kutamka zitaletwa pamoja wakati wa kutamka kama zinashikana lakini hazishikani zinakwaruzana tu,na hewa ikasukumwa kupitia mle ikasikika kama inakwamizwa/inakwaruzwa, sauti hizo huitwa
sauti za konsonanti za vikwamizo/vikwaruzo.
sauti hizi ni:/f/,/v/,/th/,/dh/,/s/,/z/,/sh/,/gh/ na /h/
iii]hewa inapozuiliwa kama ilivyo kwenye vipasuo kisha ikaachiliwa kwa mpigo lakini ikitoka ikasikika inakwamizwa,tunapata sauti za konsonanti za vipasuo-kwamizo ambapo ni moja tu katika kiswahili / ch/
iv]Hewa inapozuiliwa hivi kwamba ala za kutamkia
mbili zinagonganagongana huku hewa ikipitia kati
tunapata sauti za konsonati za vimadende.
katika lugha ya kiswahili kimadende ni kimoja tu na ni pale /r/
v]pale ambapo hewa inazuiliwa na kidakatonge na kaakaa laini kupitia kinywani na badala yake kuelekezwa puani,suati ambazo zitatamkikia puani huitwa sauti za konsonati za puani ama nazali/ving'ong'o
sauti hizi ni:/m/, /n/, /ny/, na /ng'/.
vi]Ikiwa hewa itazuiliwa na kulazimishwa kugotagota kwa ulimi kwenye ufizi na hewe hii kuachiliwa kupita pembeni mwa ulimi huo, tunapata sauti za konsonanti za vitambaza ambapo ni moja katika lugha ya kiswahili /l/.
vii]iwapo wakati wa kutamka konsonanti, hewa haitazuiliwa kama ilivyo kwenye vikwamizo lakini si huru kama ilivyo kwenye irabu tunapata sauti za konsonanti za nusu irabu au viyeyusho.
sauti hizi ni pamoja na /w/ na /ya/.
b]mahali hewa inapozuiliwa.
Pale hewa inapozuiliwa hutusaidia kuanisha sauti kwa kuziitanisha na mahala pale au ala ile ya kutamkia.
hewa ikizuiliwa kwenye midomo kwa mfano wakati wa kutamka, sauti hiyo itajulikana kama sauti ya midomoni.
hivyo sauti za midomoni,menoni,ufizini,kaakaa gumu na laini, na hata mapua, ni sauti ambazo hewa huzuiliwa hapo wakati wa kuzitamka.
ala ya kutamkia sauti midomo /b/ ,/p/,/m/, na /w/
meno /dh/ na /th/
midomo meno /f/ na /v/
kaa kaa gumu /ch/,/j/,/ny/,/k/ na /sh/
ufizini /d/,/l/, /n/ ,/r/,/t/, /s/ na /z/ kaakaa laini /g/,/gh/ na /ng'/
koromeo /h/
c]mtetemeko kwenye nyuzi za sauti
sauti yaweza aidha kusababisha mtetemeko/msepetuko/ugunaji katika nyuzi za sauti wakati wa kutamka au ikawa haina ugunaji/haisababishi msepetuko.
Iwapo itasababisha ughunaji sauti hii hujulikana kama sauti ghuna.
Mfano:I)kimadende
ii)kitambaza
iii)viyeyusho/Nusu irabu
iV)ving'ong'o
Iwapo hamtakuwa na ughunaji katika sauti kwenye nyuzi za sauti,sauti zile huitwa sauti hafifu ama sisoghuna.
Mfano:i)vipasuo.
ii)vikwamizwa/vikwaruzwa.
iii)vipasuo kwamizwa.
zoezi
Onyesha sauti ghuna+ na sisoghuna/ghuna- za luggha ya kiswahili.
Onyesha sauti ghuna+ na sisoghuna/ghuna- za luggha ya kiswahili.
SIFA ZA SAUTI ZA KONSONANTI ZA KISWAHILI
Sifa za konsonanti hutokana na vile vigezo maalum vya kuzianisha.
i)mahali inatakiwa
ii)jinsi hewa inavyozuiliwa
iii)mtetemeko katika nyuzi za sauti
Hivyo unapohitajika kutoa sifa ya konsonanti yoyote jifunge kwenye vigezo hivi.
Kwa mfano:
Toja sifa mbili za sauti /b/
a) Ni sauti ya midomoni.(mahali)
b) Ni kipasuo.(jinsi hewa inavyozuiliwa)
c) Ni sauti isoghuna.(ughunaji)
Konsonanti agharabu maswali yake hujikita katika sifa,muainisho na ughunaji.
Ili mtahiniwa kushugulikia maswali haya Ni busara kuelewa muainisho wa konsonanti kwa kuzingatia vigezo vile vitatu vya kimsingi.
Tan:
i)lazima sauti ziandikwe kwa herufi ndogo na zifungiwe kwenye mishazari.
ii)Tunatumia midomo yote miwili(lips) katika utamkaji sio midomo mmoja kutamka sauti za midomoni.
Comments
Post a Comment