Bahari za ushairi
Bahari za ushairi ni nyanja pana mno na huwa tunajikita katika vigezo vingi tu, ili kuyaainisha mashairi kibahari.
Katika Kiwango hiki, lengo likiwa kuwahi alama MBILI au NNE zikizidi sana, tutajikita katika vigezo vichache tu ambavyo lazima vijitokeze katika ushairi wowote wa kiarudhi.
Vigezo hivi ni pamoja na:
1. Bahari kutokana na vina.
i). Bahari ya mtiririko
# Vina vya ndani na nje kutiririka,kutoka juu hadi mwisho.
1 .............ta,...........pa
.............ta,...........pa
.............ta,...........pa
2 .............ta,...........pa
.............ta,...........pa
.............ta,...........pa
(Katika beti zote)
ii). Bahari ya ukara
#Mfululizo wa vina vya nje vya ndani vikibadilika.
1...........ta,.........la
...........pa,........la
...........ka,........la
2...........sa,.........la
...........wa,........la
...........ta,..........la
(Vivo hivo katika beti zote)
iii) . Bahari ya ukaraguni
#vina kubadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
1. ...........ta,..........pa
...........ta,..........pa
...........ta,..........pa
2. ...........sa,..........ta
...........sa,..........ta
...........sa,..........ta
iv).bahari ya masivina
# vina kubadilika kutoka Mishororo mmoja hadi mwingine.
1. ...........cha,.........la
............pa,..........ma
............la,............mwa
2. .............ya,.............sa
.............sa,..............tu
..............ki,..............po
Comments
Post a Comment