Skip to main content

Posts

Featured

UHURU WA MSHAIRI KATIKA USHAIRI WA KIARUDHI

Huu ni ule uwezo/ruhusa ya mshairi kutozingatia sheria za lugha ya nathari/mfululizo. Uhuru huu husaidia katika kuleta 1.usawa wa kimizani 2.mtiririko wa vina au muwala         wa vina #Uhuru huu hujitokeza kupitia     i) kuboronga sarufu.  Hali ya kutozingatia taratibu za sarufi k.v kupangua mpagilia wa sentensi wa KN na KT. ii) utohozi Kuswahilisha maneno kutoka lugha zingine kama vile kiingereza -soksi,blanketing n.k iii) Tabdila  Kubadilisha silabi ya mwisho ili kustawazisha urari wa vina bila kuathiri mizani. iv) Inkisari    Kupunguza idadi ya silabi ili kustawazisha mizani. Mfano Nimemuona aliyenipenda - memuona alonipenda. v) Mazida/Mazda . Kurefusha/kuongeza silabi katika neno ili kusawazisha mizani. vi) kikale.  Matumizi ya msamiati wa zamani ambao umesahaulika  Maninga badala ya macho.

Latest posts

4.Bahari kutokana na urefu wa mishororo

TONI KATIKA USHAIRI

3.Bahari kutokana na vigao/pande za mshororo.

2.Bahari kutokana na mpangilio wa maneno.

Bahari za ushairi

Aina za ushairi

KIIMBO KATIKA KISWAHILI

SHADDA NA KIIMBO KATIKA KISWAHILI

SAUTI ZA KONSONANTI NA MUAINISHO WAKE.

SAUTI ZA KISWAHILI NA UTAHINI WAKE